KARIBU KATIKA SOMO LA LEO. NA ASANTE KWA TUTEMBELEA BLOG HII MPYA YA OBBY MJUZI. hii ni blog maalum kwaajili ya mambo ya computer tu hii ni kutokana na maoni ya watu wengi kusema wamekuwa wakipata shida kuyaona masomo ya COMPUTER kwakuwa yanakuwa yamechanganyikana na mambo ya mziki kwenye blog yangu ile ya obbymjuzi.blogspot.com. blog ile itabaki ya mambo ya mziki na burudani. leo nitakwenda kufundiisha somo la jinsi ya kutengeneza folder ambalo huwezi kulifuta.
kuna wakati unahifadhi vyako na watu wanafuta either kwa kujua au kwakutokujua. sasa hii itakuwa msaada mkubwa sana kwenu. fata hatua hizi rahisi na utakapokwama nitumie email kupitia email yangu itmjuzi@gmail.com. PIA USISAHAU KU SUBSCRIBE HAPO JUU ILI KILA NINAPOWEKA SOMO JIPYA UTUMIWE EMAIL......
1. bonyeza windows button na R kwa pamoja. au nenda sehem ya kusearch na uandike RUN, select na kuandika CMD.
2.chagua LOCAL disk unayotaka kutengeneza hilo folder. ila usichague DRIVE ambayo ina windows (mfano local disk C).
3. kama unataka kutengeneza folder lako kwenye local disk D andika D: then ENTER.
4.then andika md con\ then ENTER
5.Hapo utakuwa tayari umetengeneza folder lako, nenda kwenye local disk lile uliloandika utalikuta limenadikwa con. unaweza kuweka kila kitu humo na hakuna mwenye uwezo wa kulifuta.
JINSI YA KULIFUTA
fata hatua hizo 3 za juu. then kwenye step ya nne andika hii rd con badala ya md con then ENTER hapo litapotea.
EmoticonEmoticon