JINSI YA KUONGEZA NAFASI (SPACE) KWENYE SIMU YAKO


Wanakwetu habari. Leo nimeona nishare nanyi somo hili dogo lakini muhim. Hii ni kutokana na maombi ya wanakwetu wengi wanaofatilia masomo yangu kupitia channel yangu ya youtube inaitwa OBBY MJUZI (ingia youtube search hivyo) au blog yangu mjuzishule.blogspot.com(tembelea humo kwa masomo mbalimvali ya computer)
Pia unaweza jiunga na darasa ninalofundisha online kwa gharama ndogo.
Utajifunza kutngeneza blog, website, graphics & designing, microsoft ofice, php,java, database, na mengine mengi.
Pia hata wewe unaweza kuuliza swali lako nami nitalijibu. Lengo ni kufanya watu wawe na uwezo katika mambo ya technology.
Watu wengi tumekuwa tukilalamika kwamba internal space ya simu zetu ni ndogo. Kuna muda tumekuwa tukiona inatuandikia memory full wakati umeweka vitu vichache tu, au muda mwingine tunataka kupiga picha na tunaambiwa 'there is no enough space' wakati ukiangalia hujaweka kitu chochote. Ukweli ni kwamba zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea memory ya simu yako kujaa mbali na kuweka vitu kwenye simu.
Leo nitaelekeza sababu mbili na njia za kuongeza zake..
1.social networks
Hii ni mitandao ya kijamii kama instagrama facebook na whatsap ila kwa kesi ya leo ntaongelea whatsap japo unaweza kutumia hata kwenye social networks zozote.
Unapotumiwa au kutuma vitu(nyimbo, voice note, videos, picha) kupitia whatsap vitu hutengeneza mafolder kwenye simu yako na kujisave huko. Hii inasababisha kitu kimoja kujisave mara mbili.
Mfano: ukituma picha kwa whatsap labda hiyo picha ilikuwa kweny folder linaitwa obby kinachotokea ni kwamba picha hiyo itakuwepo kwenye hilo folder na kwenye folder lingine la whatsap. Hivyo kama picha ina mb 2 maana yake itakuwa mb 2 kwenye folder moja na mb 2 kwenye folder lingine.
_Chakufanya_
1.nenda kwenye file manager then whatsap then media then whatsap images then utaona folder limeandikwa sent futa hilo lote.
2.rudi nyuma kisha chek whatsap audio then sent futa hilo pia
3.rudi nyuma then whatsap video then sent futa hilo pia.
4.whatsap voice note, ndani unaweza kukuta mafolder mengi futa yote.
5.then rudi mpaka kwenye media utaona neno database futa hilo lote.(usipoliona hamna shida)
6.ni muhm kufuta videos na audios na na picha ulizotumiwa kama unaona hazina umuhm au umeshazitazama. Hizo unaweza zifuta kupitia kwenye gallery.
*NOTE*
Njia hii unaweza itumia kwenye social networks zote maana kila moja inafile lake.
*2.tempolary files*
Hizi ni files ambazo huwez ziona kirahisi kwenye simu , lakini ni ukweli kwamba huwa zinachukua asilimia kubwa ya sim yako.
Hizi pia hupunguza speed ya simu yako na kuifanya iwe slow.
Hizi zinaweza kuondolewa kwa app.
Nenda playstore download app inaitwa clean master then fata maelekezo.
Kama hutumii playstor nenda kwenye source nyingne kama market.
*ASANTE*
Imeandaliwa na
*OBBY MJUZI ©2016*
```*watu makini*```
Obbymjuzi@gmail.com
Previous
Next Post »