MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER


Asante kwa kutembelea blog yangu. asante kwa kuungana nami kwenye darasa la leo. hili swali limeoulizwa na mmoja wa wafatiliaji wa masomo yangu kwamba akitaka kununua computer aangalie vitu gani? kiukweli kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla hujanunua computer(iwe desktop au laptop) iwe mpya au ya zamani. leo nitaongelea mambo makuu matatu ambayo ni muhimu sana kuyazingatia kabla hujanunua computer. yafuatayo ni mambo muhimu sana ya kuzingatia.

1. UKUBWA LA RAM
nendo ram ni kifup cha neno RANDOM ACCESS MEMORY. kazi kubwa ya RAM ni kuisaidia computer kufungua mafile na mafolder mbalimbali, pia hufihadhi taarifa kwa muda mfupi na taarifa hizi huwa zinafutika pale tu unapozima computer na kuwasha. ili computer iwe faster au iwe slow hutegemea sana ukubwa wa RAM. ndio maana RAM isipokuwepo kwenye computer yako haiwezi kuwaka, itaishia kuonesha charge inaingia lakini haiwaki.  kwahiyo unapotaka kununua computer hakikisha RAM inakuwa na ukubwa wa atleast 2GB

2. UKUBWA WA PROCESSOR
Processor ni kama ubongo wa computer yako, kitu chochote kinachofanyika kwenye computer processor ndio hufanya kazi hiyo. yan mfano unabonyeza herufi M na inatokea, kitendo hiki cha kubonyeza na kutokea huwa kinafanywa na PROCESSOR. kwa jina lingine processor huitwA CENTRAL PROCESSING UNIT. kwahiyo unapotaka kununua computer ni muhimu kuhakikisha processor yako inaukubwa kias, atleast kuanzia 2GB.

3. UKUBWA WA HARD DISK
hard diski ndio memory ya computer yako. humo ndio huhifadhiwa vitu vyote unavyoviweka kkwenye computer, mfano unapoweka mizki au movies au mafile yako yote huhifadhiwa kwenye HARD DISK, kwa kifupi huwa inaitwa HDD. ukubwa wa HDD HUTEGEMEANA NA MATUMIZI YA COMPUTER HUSIKA. kama unamatumizi makubwa nunua computer yenye HDD kubwa. na kinyme chake ni sahihi.

NB

yapo mambo mengi ya kuzingatia kabla hujanunua computer hayo niliyoelezea ndio muhim zaid na nirahisi kuyatambua, pia kama ni laptop ni vema ukajua charge inakaa masaa mangapi kabla hujaiununua.

ninaamini somo hili litakuwa msaada kwako ulieuliza pia kwa wasomaji wengine kwani wengi wamekuwa na tatzo kama hili asante.
ASANTE SANA


SOMA HII NI MUHIMU

jiunge na ONLINE CLASS ili ujifunze masomo mbalimbali kwa njia ya video hatua kwa hatua, hapa utajifunza kuelewa sio kukariri kama hujaelewa unaruhusiwa kuuliza swali lolote nasi tutakujibu lengo ni kwenda kinyume na elimu ya Tanzania inayowatengeneza watu kukariri badala ya kuelewa.(walioshiriki awamu ya kwanza watakuwa mashahidi wa hiki ninachosema). hauhitaji kuwa online muda wote ili kujiunga na somo hili. kama hautakuwa online tutakutuumia masomo kwenye email yako na utayafatilia kwa muda unaoutaka in case hujaelewa utauliza. kwasasa tumeanza awamu ya pili ya somo la JINSI YA KUTENGENEZA BLOG, gharama ya somo hili ni TSHS20,000.
KUMBUKA kwenye online class hamna hamna kuchelewa, ukianza leo tutakupa video za masomo ya nyuma na usipoelewa utauliza ili tuweze kwenda sambamba....
Pia tunaendelea na somo la HTML.
kama unahitaji kujiunga tafadhari wasiliana nami kwa email yangu obbymjuzi@gmail.com
 WAPE TAARIFA NA WENGINE

Previous
Next Post »

6 comments

Write comments
June 11, 2016 at 1:30 AM delete

Windows zote no bora ila inategemea wewe unajua kutumua vizuri window gani walio wengi hupenda seven lakini window utakayopenda jitahidi iwe na 64bits

Reply
avatar
OBBY MJUZI
AUTHOR
June 11, 2016 at 4:05 AM delete This comment has been removed by the author.
avatar
OBBY MJUZI
AUTHOR
June 11, 2016 at 4:06 AM delete

ubora wa windows hutegemea na matumizi husika, seven inaweza itwa bora zaidi kutokana na kwamba haisumbui na haina tabia ya kufa kirahisi, pia 64bts ni kitu mihim sana kuangalia unapotaka kuweka windows kwasababu software nying zinazotoka huja kwaajili ya hii tu.

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
March 8, 2017 at 2:45 AM delete

Hi, MJUZI. Naitwa Amimu Issa niko Muleba Kagera.

Kwanza napenda kuna kukushukuru kwa Darasa lako ambalo umekuwa ukitoa.

Shida yangu ni kuwa nilijaribu kufuatilia lile somo lako la JINSI YA KUFANYA KOMPUTA YAKO IFUNGUE KWA KUTAJA JINA LAKO. shida niliyokuwa nayo ni kuwa nimekuwa nikifuatilia hatua kwa hatua, lakini kwa kila nikijaribu kupaste ile username ambayo nimeandika inakataa na inaniandikia massege kuwa "You nee pamission to this Action. Naomba msaada wako kaka!!!

Reply
avatar